Kesi yao inalenga kupinga makubaliano hayo ya baada ya uchaguzi ambayo yalitiwa saini Ijumaa iliyopita na kuwasilishwa kwa msajili wa vyama vya kisiasa na Hillary Kosgei. Wakati uo huo, naibu katibu mkuu wa chama hicho Caleb Kositany alimuandikia barua ya lalama msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu akitaja kama yasio halali makubaliano kati ya chama cha Jubilee na kile cha KANU .
Kositany amesema kamati kuu ys kitaifa inayosimamia Jubilee haikukutana ili kuidhinisha mkataba huo na hivyo basi haufai kukubaliwa kwa mujibu wa sheria za vyama vya kisiasa .
Kositany amesema makubaliano hayo ni ukiukaji wa sheria kwani utaratibu ufaao wa kisheria haukufuatwa. Siku ya Jumanne jopo la kusuluhisha mizozo ya kisiasa lilikizuia chama cha Jubilee kutekeleza mkataba wake wa muungano na chama cha Kanu.