Wabunge hao wamesema rais anafaa kutekeleza matakwa ya katiba aliyoapa kufuata kwa kulivunja bunge ili kuwezesha uchaguzi kuandaliwa . wamesema pia kwamba wako tayari kuzitetea nafasi zao
Miongoni mwa wabunge waliotoa wito huo kwa rais ni mbunge wa Kuria magharibi Mathias Robi ,Charles Gimose wa Hamisi miongoni mwa wengine wakati walipokuwa wakiwahutubia wananchi katika eneo bunge la Bumula ,huko Bungoma .
Mbunge wa Gatudu Kusini Moses Kuria aliwashauri kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na Moses Wetangula wa Ford Kenya kukoma kuwapeleka wakenya katika upinzani.
Amesema mrengo unaomuunga mkono Ruto utaunda serikali ijayo na hataki watu wa eneo la magharibi kujipata katika upande wa upinzani .
Mbunge Gachagua Nderitu wa Mathira alimshambulia katibu mkuu wa muungano wa COTU Francis Atwoli akisema kwamba Atwoli haiwakilishi jamii ya Waluhya .