1894425

Washukiwa sita wazuiliwa kwa kifo cha mwanaharakati Carolyne Mwatha

Washukiwa sita waliohusika na kifo cha mtetezi wa haki wa Dandora Carolyne Mwatha watazuiwa kwa siku 14, uchunguzi ukiendelea,

Michael Onchiri, Betty Akinyi, Richard Ramoya, Alexander Gikonyo, Georgia Achieng, na Stephen Maina watazuiliwa hadi wakati uchunguzi wa kifo utaisha.

Utamaduni huniruhusu kusherekea siku ya wapendanao (Valentine) – Nasra

Inspekta Joseph Wanjoi aliliambia mahakama ya Makadara washukiwa hao walishikwa jumanne katika maeneo ya Dandora kisha kupelekwa katika kituo cha polisi cha Buruburu.

Washukiwa hao wako chini ya uchunguzi na wengi ambao bado hawajashikwa wako mafichoni, lakini wanasahu kuwa mbio za nyani huishia jagwani.

1894425

“Mimi na timu yangu ya uchunguzi hatujaweza kuchanganua rununu ambazo waashukiwa hao walikuwa wanatumia wakati wa tukio hilo,

“Nguo ambazo walikuwa wamevalia na silaha ambazo walitumia wakati huo na utambulisho wa washukiwa hao haujafanyika,”Joseph aliambia mahakama.

‘Stand true to your calling…’ Ruto’s first born son, Nick, makes his father proud!

Aliweza kuwaonya kuwa washukiwa hao wanaeza ingilia mashahidi, ama wakiweza kuachiliwa kwa dhamana, familia na mawakili wao tu ndio wataweza kuambiwa kuwahusu.

Joshua Ochieng’
Joshua Ochieng’

Wahusika hao walikana mashataka hayo na kusema kuwa watashirikiana na mahakama wakiweza kuachiliwa kwa dhamana.

“Mimi ni mgonjwa na siwezi kimbia polisi, na tayari polisi wanajua mahali tunaishi kwa hivyo hakuna haja ya kutuzuilia,” Alisema Akinyi.

Lakini hakimu mkuu wa mahakama ya Makadara Heston Nyaga alisema kuwa washukiwa hao wana haki ya katiba ya kuachiliwa na dhamana, katiba kuwa inakubali waweze kuzuiliwa kwa maana wamekamatwa na mashtaka mabaya, na kusema kuwa Akinyi aweze kupelekwa hospitali kwa matibabu.

 

caroline mwata 1

Kesi hiyo itatajwa Februari 27, DCI alisema kuwa Caroline alifariki akijaribu kuavia mimba, katika kliniki moja eneo la Dandora phase1, na kuwa washukiwa hao wanaweza kuwa wanaweza kuwa waliwezesha au walishiriki katika kisa hicho.

“Februari 6 Carolyne aliweza kuenda katika kliniki moja Dandora (New Njiru Community Centre) phase 1,

“Inaaminika kuwa kuavia kwa mimba hiyo kulifanywa na mwenye kliniki hiyo Betty Akinyi almaarufu Betty Ramoya, na daktari mmoja ‘Dkt’Michael Onchiri almaarufu Dkt Mike,” DCI George Kinoti alisema.

Aliweza kuongea na kusema kua wachunguzi wanaamini kuwa Caroline aliweza kufariki baada ya kuavia mimba katika kliniki hiyo, kisha mwili wake kupelekwa katika nyumba ya kuifadhi maiti ya Nairobi saa 4:42 asubuhi.

Protests held over delay in releasing Caroline Mwatha’s autopsy report

Kinoti alisema kuwa kupotea kwa Caroline kuliweza kuripotiwa Ijumaa katika kituo cha polisi cha Dandora. Alisema kuwa rekodi za chumba cha kuifadhi maiti inasoma kuwa Mwili huo uliweza kupelekwa na gari ambayo ina namba ya usajili KBP677B.

Polisi walisema kuwa Gikonyo ndiye alikuwa na jukumu la ujauzito wa mwezi mitano wa Caroline, na kuwa wachunguzi waliweza kusema kuwa Gikonyo aliweza kumtumia Caroline shillingi 6,000 za kuavya mimba.

Mume wa Caroline, Joshua Ochieng anafanya kazi Dubai, na Caroline walikuwa wakiongea kwa sana na Gikonyo kabla ya madai ya kuavia mimba.

 

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments