Washukiwa wa wizi wa boda boda wachomwa

Washukiwa watatu wa wizi wa pikipiki mjini Voi kaunti ya Taita Taveta wameteketezwa na umma hadi kufariki baada ya kutiwa  baroni na waendeshaji pikipiki mjini humo.
 
Mmmoja kati yao aliyenusuriwa na polisi alifariki alipokuwa anapelekwa kupokea matibabu mjini Mombasa.
 
Akithibitisha kisa hicho kamishena wa kaunti Josephine Onunga ameonya umma dhidi ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake akawataka kutoa ripoti kwa polisi ili kusaidia kukamatwa kwa washukiwa wote.