Washukiwa wanne wa shambulizi la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa kuhukumiwa leo

Washukiwa wanne wanaoaminika kuhusika katika shambulizi la kigaidi katika  chuo kikuu cha Garissa watajua hatama yao hii leo mahakama itakapo toa hukumu. Walipatikana na makosa uuaji, kuwa katika kundi la kigaidi na kutekeleza shambulizi katika chuo hicho.

Shambulizi hilo la Aprili 2, 2015 liliwaacha watu 148 wamefariki  huku watu zaidi ya 79 wakiachwa na majeraha.

Magaidi waliotekeleza shambulizi hilo waliwateka nyara zaidi ya wanafunzi 700, kuwaacha huru waislamu na kuwauawa wa kristo.

Magaidi wote wanne waliotekeleza shambuli hilo waliuawa na wanaume watano kukamatwa baadaye kwa madai ya kuhusika katika kupanga shambulizi hilo.