nameless

‘Wasichana msidanganywe na wanaume wa six pack,’Nameless awaonya wasichana

David Mathenge almaarufu Nameless kwa muda amekuwa akitoa maoni yake kwenye mitandao ya kijamii, huku akiwashauri mashabiki wake.

Kama baba wa wasichana ambao wamo katika umri wa ujana wao hajaacha wasichana na wanawake kuanganywa na wanaume ambao hawamo tayari kuingia katik uhusiano wa kimapenzi na wao.

‘Hufikiri ni wakati wakumpata mvulana, shabiki amuuliza Nameless huku akijibu

Kupitia kwenye mitandao yake ya  kijamii ya instagram Nameless aliposti video akicheza akiwa chumbani chake chaa kulala na kwa mara ya kwanza alionyesha kifua chake.

 

Baada ya kupakia video hiyo aliandika ujumbe akiwaonya wasichana dhidi ya kupenda wanaume wenye kifua kikubwa wakidhani ya kwamba wana pesa.

“Wanaume wa one pack mpo? wasichana msidanganywe na wanaume wa six pack, hawakuangi na pesa akiba yao yote huenda kwa gym na chakula 

Jipatie mwanamume wa one pack.” Aliandika Nameless.

‘Kwani huyu mrembo wetu ni ngori? Mashabiki wamuuliza Nameless baada ya kufichua hulala kwa kiti

Kutokana na video hiyo Nameless anaonekana kujua hatua na kufahamu hatua za kucheza, msanii huyo na mkewe Wahu walifunga pingu za maisha mnamo mwaka wa 2005.

 

 

Photo Credits: maktaba

Read More:

Comments

comments