Watoto baraka! Picha za nyumba ya mamake Betty zapendeza macho

Betty Kyallo ni mfano mzuri sana wa msemo, mchumia juani hulia kivulini kwani binti huyu ambaye ni mtangazaji maarufu wa televisheni ya K24 ameweza kupata cheo cha watangazaji bora nchini kupitia kwa kazi yake maarufu.

Kidosho huyu alianza kufanya kazi katika kampuni ya Media Max hivi juzi tu baada ya kufanya kazi kwenye kampuni ya Standard Media Group kwa miaka zaidi ya minane.

Tangu binti huyu aende kwenye runinga ya K24 ofisi za humu zimejawa na furaha si kidogo kwani kitengo cha binti huyu cha Weekend with Betty kimeweza kupata mashabiki wengi sana kutoka hapa nchini na hata mashabiki wa nchi jirani.

Katika mahojiano ya hivi juzi na mpasho.co.ke, Betty alisema,

WORKING AT K24 HAS BEEN SO REFRESHING. IT WAS INDEED THE RIGHT CHOICE ESPECIALLY AFTER BEING AT KTN FOR 8 YEARS. I’VE MADE NEW FRIENDS, NEW AMAZING CONTENT AND NEW AUDIENCES. I’M HAPPY AND COMPLETELY SETTLED. PAT ON MY BACK,’

Hivi juzi alifanyiwa mahojiano katika nyumba ya mamake mzazi na ilikuwa wazi kuwa mama yake anaishi maisha mazuri sana,yaani maisha ya kifalme.

Tazama picha usadiki kuwa,mamake Betty Kyallo anais