Watoto wangu 3 wamekwama China !

China
China
Baba ya  wanafunzi watatu wa Kenya ambao wapo nchini China ameeleza masaibu anayopitia  kwa ajili ya  kuzuka kwa virusi vya Corona na kuwazuia wanawe kurejea nchini .

Kufikia sasa virusi hivyo vimesababisha vifo vya watu 2000 kote duniani  huku zaidi ya elfu 15 katika taifa la China wakiambukiwa .Frankline Olumasai  kutoka  Kitui  ameeleza jinsi alivyopatwa na mawazo kupindukia na kukosa matumaini ya kuwaona watoto wake wakato ugonjwa huo ulipozuka katika mji wa Wuhan .

".... Binti yake alinipigia simu kuhusu kufungwa kwa mji huo ,na hapo ndipo maibu yangu yalipoanz’ Olumasai amesema .

Olumasai  amesema watoto wake hao wawili wa kiume na mmoja wa kike  wapo China kwa masomo ya kujifadhili .

"...  Kwa sasa tuko sawa lakini binti yangu amezuiwa kuonndoka mji wa Wuhan .vijana wangu wawili  walihamia mkoa mwingine’ amesema .

" Nilijaribu kuwapigia simu rafiki zangu walio  China wajaribu kumsaidia binti yangu lakini  tulichelewa kumsaidia aondoke Wuhan’. Wakenya wamehamakishwa na hatua ya serikali kuruhusu ndege moja ya China kuingia nchini ikiwa na abiria zaidi ya 200 ilhali wanafunzi kadhaa waliokwamna Wuhan waliotaka kurejea nyumbani hawajasaidiwa .