Idadi ya sampuli zilizopimwa sasa ni 532,729. Visa vyote ni vya wakenya isipokuwa vinane.159 ni wauame ilhali 59 ni wanawake .Mgonjwa wa umri wa chini sana ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 78 .
Nairobi ndio inayoongoza kwa visa 68 ikifuatwa na Kisii 28,Mombasa 21,Kisumu 19,Kimbu 13 Kajiado 11,Busia 10,Machakos 8,Tharaka Nithi 6 ,Garissa 6, Taita taveta visa 5 Nakuru visa 4 ,Uasin Gishu visa 3,Narok visa 2,Laikipia visa 2 Kakamega visa 2,Kericho visa 2, Murang’a,Bomet,Kilifi ,Migori ,nyandarua na Nyeri zina kisa 1 kila moja.
Watu 170 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 24,504 idadi ya wote waliopona corona nchini hadi kufikia sasa .
Leo watu 13 wameaga dunia na kufikisha 682 watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo .