Watu 13 waliojumuika na mwathiriwa wa Corona wawekwe kwenye karantini

EXfqPJEXQAABjiz
EXfqPJEXQAABjiz
NA NICKSON TOSI

Watu kumi na watatu waliotakutana ama kujumuika na mwathiriwa wa virusi hatari vya Corona katika kaunti ya Isiolo wamewekwa chini ya karantini.

Waziri wa afya kwenye kaunti hiyo Ibrahim Alio amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kubaini iwapo jamaa hao waliambukizwa virusi hivyo.

Kaunti ya Isiolo imekuwa ya hivi karibuni kusajili kisa cha virusi hivyo na kuwafanya wakaazi wa eneo hilo kuwa ange.

Yakijiri hayo ya corona ni kuwa familia ya marehemu Njenga Karume imepata afueni baada ya mahakama kuondoa majina ya watu watatu waliokuwa wanatarajia kunufaika na ugavi wa mali aliyoacha mwanabiashara huyo.

Mahakama imetoa majina ya watu hao watatu almaarufu kama trustees ili kuipa familia kupata njia mwafaka ya kusuluhisha mgao wa mali hiyo.

Mkusanyiko wa taarifa awamu hii