Watu 133 wamepatikana na virusi vya corona- Mutahi Kagwe

Eaol0HTXQAA76SO.jfif
Eaol0HTXQAA76SO.jfif
Waziri wa afya nchini amesema kuwa baada ya kuwafanyia watu 3,255  vipimo watu 133 wamepatikana na virusi huku waathiriwa hao wote wakiwa wakenya.

Takwimu hizo mpya sasa zinafanya taifa la kenya kuwa na watu 3,860 walioambukizwa virusi hivyo.

Wanume kati ya visa hivyo vipya ni 88 huku wanawake wakiwa 45.

Serikali pia imewaruhusu watu 40 kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na idadi ya waliopona virusi hivyo kufikia watu 1326.

Mgonjwa mmoja ameripotiwa kufariki kutokana na virusi hivyo na kufikisha watu 105 waliofariki hadi sasa.

Visa hivyo vipya vimetokea maeneo yafuatayo nchini, Mombasa 61, Nairobi 53,Kilifi 7, Busia 6, Kiambu 2 na Kajiado, Nakuru, Murang'a na Kitui kimoja.

Wakati uo huo Mutahi ameongezea mikahawa nchini muda wa kufanya biashara hadi saa 7:30 usiku japo akaongezea kuwa ni sharti usimamizi wa mikahawa hiyo kuhakikisha kuwa wafanyakazi wake wanapimwa.