Watu 134 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa- Mwangangi

EZv11ABWkAAWHV-
EZv11ABWkAAWHV-
Katibu msimamimizi katika wizara ya afya nchini Mercy Mwangangi amesema kuwa watu wengine 134 nchini wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwaa vipimo.

Visa hivyo vipya sasa vimefikisha watu 2,447 nchini walioathirika na virusi hivyo.

Wakati uo huo, Mwangangi amesema serikali imewaruhusu watu 51 kutoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 643.

Miongoni mwa visa hivyo vipya hii leo, kaunti ya Mombasa imesajili watu 69, huku kaunti ya Nairobni ikisajili visa 31.

Mwangangi aidha amesema mgonjwa mmoja amefariki kutokana na virusi hivyo hatari na kufikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo kuwa 79.

Wanaume ni 98 na wanawake 36 katika visa hivyo vipya 134 ambavyo vimesajiliwa hii leo.

Wakatai uo huo Mwangangi amewataka wakenya kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali ili kupunguza maambukizi ya visa hivyo.

Kulingana na visa ambavyo vimeripotiwa katika kaunti ya Busia, Mwangangi amesema watu hao wote ni madereva ambao walipimwa baada ya kuwasili nchini.

Ameongezea kuwa maafisa wa afya wamepelekwa katika makaazi ya wakimbizi ya Daadab kuanza kuwapima watu hao baada ya kuripotiwa kuwa waathiriwa wa virusi hivyo.

Ameshikilia wazo kuwa serikali itakuwa inawaruhusu baadhi ya wagonjwa kutoka kwa hospitali humu nchini ili kushughulikiwa nyumbani kutokana na hatua ya hospitali hizo kuanza kujaa.