Watu 181 wapatikana na virusi vya corona

Imebainika kuwa baada ya sampuli za watu 2,131 kufanyiwa vipimo,watu 181 kati yao wamepatikana na virusi vya corona na kufanya taifa kuwa na watu 8,067 walioathirika na virusi hivyo.

Wakati uo huo watu 127 wameruhusiwa kuondoka hospiatlini na kufikisha watu 2, 414 waliopona dhida ya virusi hivyo.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo imefikia watu 164 naada ya watu wanne zaidi kufariki.

Kati ya visa hivyo vipya ,Nairobi imesajili visa 134, Kiambi - 19 Mombasa - 9 Kajiado na Machakos - 6 ,Lamu - 3, Murang’a - 2 ,Yasin Gishu na Kiriyaga - 1 .

Kufikia sasa Kenya imewapima watu 191,394 kuhusiana na virusi hivyo.