Watu 213 wamepatikana na virusi vya corona nchini- Aman

Kenya sasa ina wagonjwa 4,257 wa corona baada ya watu wengine 213 kupatikana na virui hivyo  baada ya kufanyiwa vipimo chini ya saa 24.

Kulingana na Aman kaunti ya Nairobi inaongoza na visa 136 huku Mombasa ikiwa na 32.

Kati ya visa hivyo vipya, wakenya ni 198, raia wa kigeni 15.

Kulingana na jinsia, Aman amesema wanaume ni 151 huku wanawake wakiwa 62.

Aman amesema kuwa watu 106 waliokuwa wameathirika na virusi hivyo wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 1,459 waliopona.

Waathiriwa hao ni wa kati ya miaka mmoja hadi 73.

Watu wengine 10 wamefariki na kufikisha idadi ya wale walioaga nchini kuwa 117.

Wakati uo huo Aman amewataka wakenya kuendelea kuwa ange kutokana na hatua ambapo virusi hivyo vya corona vinaendelea kusambaa nchini.

Amewataka wakenya kuendelea kuheshimu masharti yaliyowekwa na wezara ya afya kama njia ya kupunguza maambukizi.