Watu 22 wapatikana na virusi vya corona kufikisha idadi kuwa 737

EX5kyj9XkAAOGa-
EX5kyj9XkAAOGa-
Katibu katika wizara ya afya Rashid Aman amesema chini ya saa 24, wamefanyia watu 1516 na 22 kati yao kupatikana na virusi hivyo kufikisha idadi nchini kuwa 737.

Kati ya watu hao 22, 21 ni wakenya huku mmoja akiwa raia wa kigeni.

Aidha serikali imewaruhusu watu 22 kutoka hospitalini na kufikisha idadi ya watu waliopona hadi 281.

Watu wanne aidha wamefariki na kufikisha idadi ya walioafariki kuwa 40.

Kulingana na Aman, kati ya watu hao 22, 17 ni wanaume na watano ni wanawake.

Aidha mtu wa umri wa chini zaidi miongoni mwa maambukizi mapya ana umri wa miaka 20.

Visa hivyo vipya vimetokea maeneo yafuatayo;

10 Nairobi, 8 Mombasa, 3 Kajiado, 1 Bomet.

Rashid amesema wanatarajia kupata kliniki tamba kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo itawekwa karibu na mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga.

Wakati huo huo Aman amewataka wakenya kuzingatia masharti yaliyowekwa ili kuzuia maambukizi zaidi.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO