Watu 31 wamepatikana na virusi vya corona Kenya- Rais Kenyatta asema

Akitoa hotuba yake kwa taifa Jumamosi,rais Kenyatta amesema wakenya wengine 31 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya watu walioathirika  nchini kuwa watu 1192.

Kenyatta amesema kufikia sasa ,taifa limewapima watu 57650 kote nchini .

Wakati uo huo kKenyatta amesema serikali yake imetenga milioni 250 kwa minajili ya watu walio na mahitaji spesheli na ambao wameathirika pakubwa kutokana na janga la corona.

Amesema kupitia mpango wa Kazi Mtaani ,vijana wengi nchini wameajiriwa na serikali chini ya kauli mbiu hiyo ili kusafisha miji yote nchini.

Ameongezea kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 5 ili kufanikisha usalishaji wa bidhaa za humu nchini na kuinua maisha ya mkenya wa kawaida.

Kenyatta amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuangazia jinis ya kurejelea shughuli za masomo nchini .

Kuhusiana  swala hilo hilo la elimu ,Kenyatta amesema wataajiri walimu 10,000 kote nchini ili kufanikisha masomo kupitia dijitali.

Hazina ya kitaifa imetenge shilingi bilioni 30 kwa minajili ya kurekebisha njia zote zilizoaribika nchini.

Kenyatta vile vile amesema serikali imetenga mikakati murwa ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.

Ameelezea kuwa serikali vile vile itawaajira wahudumu wa afya kutoka kwa kitengo cha stashahada na shahada ili kufanikisha shughuli za matibabu.

Kuhusiana na sekta za Utafiti nchini,Kenyatta amesema serikali imetenga pesa za kutosha ili kufanikisha utafiti katika idara hizo.

Kuhusiana na kilimoi.Uhuru amesema serikali itahaklikisha imepunguza bei ya mbolea ili kuwapa wakulima wakati wa kujianda upanzi.

Wizara ya Utalii nchini imetengewa shiliongiu bilioni moja kama njia ya kuinua kiwango cha Utalii nchini ambacho kimeathirika pakubwa .

Serikali imetenga shilingi milioni 600 ili kufanikisha ununuzi wa vifaa ambavyo vinatengenezwa nchini chini ya kauli mbiu buy kenya built Kenya.

Kenyatta ameira bunge la kitaifa kupitiusha mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu ili kufanikisha maisha ya mkenya wa kawaida.

Shiulingi bilioni 1.7 zimetengwa kwa minajili ya kupanua hospitali za humu nchini.

Kiongozi wa gtaifa amesema kuwa serikali pia imetenga bilioni 10 ili kulipa madeni yake yote.

Bilioni 1.5 zimetengewa wakulima wa kilimo cha mauwa nchini ili kujikimu kimaisha baada ya biashara zao kusitishwa kutokana na hatua ya serikali nyingi kufunga shughuli za usafiri.

Amewatakia waislamu wote siku njema ya kufungua mfungo wa Ramadan japoa akawakumbusha kuheshimu masharti yaliwekwa na serikali.

Kenyatta amewataka wakenya kuendelea kushirikiana na serikali kama njia ya kuangamiza kabisa janga la corona