Watu 32000 wapona corona Afrika -WHO

Takwimu kutoka shirika la afya duniani tawi la Afrika ni kuwa kufikia sasa watu 32000 wamepona virusi hivyo huku walioaga dunia wakiwa 2700.

WHO pia imesema kuwa maambukizi katika bara la Afrika yanaendelea kuongezeka huku watu 84000 kufikia sasa wakiwa wameambukizwa virusi hivyo.

Taifa la Afrika kusini mbali na kufungua baadhi ya biashara,linaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi likiwa na watu 15,515 walioambukizwa virsui hivyo .

Mataifa kama Misri na Algeria yangali na idadi kubwa ya watu walioafariki yakiwa na 612 na 548 mtawalia.

Kenya kufikia sasa imeandiksha visa 887 vya maambukizi huku watu waliopona wakiwa 313 kufikia sasa.