Watu 7 zaidi wamepatikana na virusi vya Corona kufikisha idadi ya walioathirika kuwa 38

kaku
kaku
NA NICKSON TOSI

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kuwa watu 7 zaidi wamepatikana na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo  na madaktari na kufikisha idadi ya watu walioathirika kuwa 38.

Kati ya watu hao 4 ni wakenya ,2 raia wa Kongo na kutoka  1 Uchina.

Visa hivyo vipya 7 vimepatikana baada ya watu 81 kufanyiwa vipimo na madaktari katika masaa 24 yaliyopita huku watu 71 wakiruhusiwa kuenda nyumabani.

Kati ya watu hao 7 ,wa 3 ni wanawake na 4 ni wanaume.

Kufikia sasa kaunti ya Nairobi inaongoza na visa  28 ,ikifuatiwa na Kilifi 6,Mombasa 2,Kajiado na Kwale zote zikiwa na kisa kimoja.

Mutahi aidha amewataka wakenya kuheshimu mikakati ambayo serikali imeweka ya kuakikisha kuwa hakuna watu wengi wanaoambukizwa virusi hivyo.

Kuanzia kesho waziri amesema wataanza kupima wanachi kote nchini kubaini idadi ya watu ambao wanaweza kuwa na vitrusi hivyo .

Waajiri pia wametakia kuwachilia wafanyakzi wao mapema ili kuwafanikisha kufika nyumbani kwa wakati kabla ya muda uliowekwa na serikali.