Watu 9 waaga dunia huku visa vipya 139 vya corona vikiripotiwa

mercy
mercy
Kenya siku ya jumanne imesajili visa 139 vya ugonjwa wa corona  na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa  37,218,  katibu wa utawala wa afya  Mercy Mwangangi  amethibitisha .

Idadi hiyo ni kutoka sampuli 1774 zilizopimw akatika saa 24 zilizopita . kati ya visa hivyo vipya 125 ni vya wakenya ilhali 14 ni vya raia wa kigeni . wanaume ni 112 ilhali wanawake wakiwa 27 .mgonjwa wa umri wa chini ana  miaka mine ilhali wa umri wa juu ana  miaka 82.

Watu 198 wamepona ugonjwa huo na kufikisha jumla ya idadi ya walipona kuwa 24,147.

Hata hivyo taifa limewapoteza watu 9 kwa ajil ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya walioaga dunia hadi sasa kuwa 659