Watu Watano waaga dunia baada ya gari lao kusombwa na mafuriko Kajiado

Kajiado Five
Kajiado Five
Watu watano wa familia moja wameaga dunia leo huko kajiado baada ya gari walimokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko  walipokuwa wakivuka daraja la  Mto  Ng’tataek  mapema hivi leo . watano hao walikuwa wakitoka sherehe ya harusi nchini Tanzania  kabla ya kumtembelea jamaa yao katika eneo la namanga . kamanda wa polisi kajiado ya kati Daudi ole Lornyokwe amesema baadaye walipokuwa wakielkeea Bissil ili kuvuka daraja hilo,gari lao lilishindwa nguvu  na maji  na kusombwa

Lornyokwe  amesema gari hilo lilikuwa limewabeba  mwanamke mmoja  na wanawe wawili  na wanaume wawili wote wa familia moja . “ Tumeshaiondoa miili yao pamoja na mabaki ya gari hilo  ma miili inapelekwa katika hospitali ya rifaa ya Kajiado’ amesema kamanda huyo wa polisi . Kamishna wa kaunti ya Kajiado Joshua Nkatha  alikimbia katika eneo la mkasa  ili kuzifariji familia za walioathiriwa na  maafa hayo .

Mvua kubwa inayozidi kunyesha katika maeneo mengi ya taifa imezidi kusababisha maafa na hasara huku zaidi ya watu 46 wakiaga dunia huko West Pokot baada ya kutokea maporomoko ya ardhi .  Idara ya utabiri wa hali ya anga tayari imesema Sehemu nyingi za taifa zitaendelea kupokea kiasi kikubwa cha mvua .idara hiyo  imesema maeneo ya kati ,magharibi  ,kaskazini mashariki  na Rift valley  yataathiriwa zaidi .wale wanaoishi katika maeneo ya  chini wameshauriwa kuhamia sehemu za juu .Kwingineko  wakaazi wa Taita Taveta  wametahadharishwa  kuhusu uwezekano wa kutokaea maporomoko ya ardhi  katika baadhi ya sehemu hiyo kwa ajili ya mvua kubwa inayoshuhudiwa .  Maporomoko madogo ya ardhi   tayari yameshuhudiwa katika  maeneo ya  Mbengonyi, Mdangenyi, Msawe  na  Mbale.