Watu watatu kuaga dunia katika ajali ya barabara Ndhiwa

Watu watatu waliaga dunia Jumatatu jioni baada ya ajali ya barabara katika maeneo ya Ndhiwa Migori,ni ajali ambayo ili waacha watu sita wakiwa na majeraha mabaya na kisha kuenda kutibiwa.

Kweli hawakukosea waliposema ajali haina kinga kwa maana abiria hao hawakujua yatakayo jiri wala wanafunzi hao hawakujua kuwa hawatatimiza ndoto zao maishani.

Wanafunzi hao wawili walikuwa wanatoka shule wakitembea kando ya barabara,walikuwa wa shule ya upili ya Ojode Pala.

Ajali hiyo ilisababishwa na Lori lililokuwa likienda kwa mwendo wa kasi ndipo likapoteza mwelekeo na kugonga gari ya abiria lililokuwa linawabeba abiria kando ya barabara.

Shahidi aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa wanafunzi hao walikuwa wanatembea kando ya barabara ndipo walipo gongwa na kufa papo hapo.

"Lori hilo lilipoteza mwelekeo kisha likaenda kugonga gari hilo la abiria, ndipo likaenda kugonga wanafunzi hao waliokuwa wakitoka shule,"Alieleza shahidi.

Lori hilo lilikuwa lime beba vifaa vya ujenzi likitoka katika mji wa sori katika kaunti ya Migori na lilikuwa linaelekea Rodi kopany.

OCPD wa ndhiwa Dishon chadaka akiongea Jumanne alisema kuwa walionusurika walipelekwa katika hospitali ya kaunti ya Homa Bay(Homa Bay referral hospital) kwa matibabu zaidi.

Walioumia ni dereva wa lori hilo na mwenzake, pia polisi walisema kuwa hawangewajua wala kuwatambua waathiriwa kwa wakati huo.

"Gari zilizoaribika kutokana na ajali hiyo zimepelekwa katika kituo cha polisi cha Ndhiwa kwa ukaguzi wakiendelea na uchunguzi zaidi,"Chadaka aliongea.

Wakazi wa Ndhiwa walilalamika kwa sababu ya mashimo yaliyomo katika barabara yanayosababisha ajali nyingi katika eneo hilo.

Zaidi ya kilomita 12 barabara haiwezi pitika kwa sababu ya mashimo hayo, Selly Manyala alisema kuwa inawabidi Madereva wa magari kutafuta njia kando ya barabara ili waweze kupita.

"Magari mingi huwa yanatafuta njia katika mashamba ya kibinafsi iliweweze kupita wakiogopa mashimo yaliyo katika barabara,"Alizungumza Manyala.

Mbunge wa eneo hilo Martin Owino aliweza kuuliza Kenya National Highway Authority kutengeneza tena barabara hiyo kwa haraka ili wazuie ajali katika barabara hiyo.

"Nawahimiza serikali waweze kujenga barabara ya Rodi-Kopany kuelekea Ndhiwa ili tuzuie watu kupoteza maisha yao na ajali katika eneo hili,'Owino aliongea.