merlin_140906961_6e0e3d89-f56b-427b-afed-582f3c0116c2-articleLarge

Watu 3 wateketea moto katika vyumba vya malazi Nairobi

Riruta fire Njambi KoikaiWatu watatu wameteketea kiasi cha kutotambulika mapema siku ya Jumatano baada ya moto kuchoma nyumba wanazoishi karibu na Bus Station, jijini Nairobi.

Polisi wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha kua moto huo ulisababishwa na mlipuko wa mtungi wa gesi na kusambaa kwa haraka.

Jamaa ashtakiwa kwa kujifanya kuwa afisa wa polisi Voi

Moto huo ulianza katika hoteli iliyopo karibu na vyumba hivyo na kusambaa kwa majengo mengine.

Wazima moto walitumwa katika eneo hilo na wakafanikiwa kuuthibiti moto huo, lakini tayari ulikua ushasababisha hasara kubwa kwa wakazi.

Ng’ang’a hana makosa kuita watu “takataka”- Gilbert Deya

Polisi wamesema waliipata miili mitatu na wangali bado wanachambua kifusi ili kuona iwapo kuna miili mingine.

Miili hio ilijumuisha ule wa mwanamke mmoja na wanaume wawili.

Eneo hilo limetengwa na wananchi hawapaswi kutembea mle hadi maafisa wa polisi watakapotamatisha shughuli za uchunguzi kuhusu kisa hicho.

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments