Watu wawili akiwemo mwanafunzi wauwawa na majambazi, Busia

Watu wawili akiwemo mwanafunzi wa shule ya msingi wameuawa na watu wanaoaminika kuwa majambazi katika kaunti ya Busia usiku wa kuamkia leo.

Katika kisa cha kwanza, mhudumu mmoja wa bodaboda amepatikana ameuawa kinyama mjini Nambale huku waliomuua wakiacha pikipiki yake mpya hatua chache kutoka kwa nyumba ya kukodisha anakoishi.

Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Nambale Robert Ndambiri amesema wameanzisha uchunguzi ili kuwatia mbaroni wahusika, huku pia akiungana na mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Gilbert Okumu kuwataka wanachi kushirikiana na maafisa wa polisi katika kuwatambua wahalifu.

Kisa cha pili, mwanafunzi mmoja mvulana wa darasa la nane kutoka kijiji cha Buriangá ameuawa kinyama na majambazi usiku wa kuamkia leo.

Matayo Nyengenye anasema mkuu wake anaeishi naye Gerephas Obonyo alikuwa anaenda Matanga katika kijiji cha Sirisia akiwa na wenzake wawili ambao pia ni wanafunzi wa darasa la nane wakati alivamiwa na watu wawili na kudungwa kisu mara kadhaa na kufariki papo hapo.

-Leonard Acharry