Watu wawili mmoja wao mwandishi wa KTN wafariki katika ajali

unnamed (1)
unnamed (1)
Watu wawili waaga dunia katika ajali mbaya ya barabara baada ya gari mbili kugongana katika barabara ya Kajiado-Namanga siku ya Jumamosi.

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari aina ya Toyota Probox kugongana na Lori iliyokuwa ikiendeshwa na raia wa Burundi katika mida ya saa kumi na mbili unusu jioni.

“Dereva wa Probox alijaribu kukwepa kugonga trela iliyokuwa imebeba mbao ikielekea Kajiado," Kamanda wa Central Daudi Lornyokwe alisema.

Lornyokwe alisema mtu mmoja kati ya wanne waliokuwa ndani ya Probox aliaga papo hapo.

Polisi walipeana jina la raia huyo wa Burundi aliyeaga kama Isidore Birigirimana (34) na Edwin Audi, alitambulishwa kama mfanyikazi wa kituo cha runinga cha KTN.

Polisi walisema kuwa walioumia walipelekwa katika hospitali ya kaunti ya Namanga kufanyiwa matibabu.