Watu wawili waponea kifo baada ya lori kuwaka moto

Dereva wa lori na msaidizi wake waliponea kifo siku ya alhamisi, hii ni baada ya gari walilokuwa wakisafiri likikumbwa na shida ya kiufundi walipokuwa wakiteremka mlima ya Subuiga kando ya barabara kuu ya Isiolo-Nanyuki.

Trela hilo ambayo ilikuwa inaendeshwa kwa kasi sana lilipoteza breki zake kabla ya magurudumu ya mbele kushika moto huku ukiingia mjini Isiolo.

Dereva alifanikiwa kupata njia ya kupita katika mji huo, huku eneo la mbele la trela hiyo ikiwaka moto. Hatimaye trela hio ilisimama baada ya kilomita moja kutoka mji huo wa Isiolo.

Hakuna mtu yeyote alijeruhiwa katika tukio hilo lakini dereva ambaye alikuwa ameshtuka kufuatia tukio hilo, alikimbizwa katika hospitali ya Isiolo referral kwa kuwa alikuwa amevuta pumzi mafusho.

Trela hiyo ilikuwa imebeba matofali ya ujenzi kutoka kaunti ya Kajiado ikipeleka Isiolo. Ben Kariithi ambaye ni mwendeshaji boda boda katika mji huo, alishuhudia tukio hilo na anasema kuwa ilikuwa tukio ambalo liliwashtua wakazi wengi.

Waendeshaji kadhaa wa boda boda walifuata trela hiyo na kuzima moto huo kwa kutumia mchanga kabla gari la kuzima moto ya kaunti hiyo ya Isiolo kuwasili na kuzima moto huo kabisa.

Kariithi aliwataka madereva wanaondesha magari barabarani kuwa waangalifu sana hasa wanapokaribia mlima wa Subuiga ambao umesababisha ajali nyingi.

Robinson Ambaisi ambaye alikuwa msaidizi wa dereva katika trela hio, alisimulia hali ya kusikitisha ya kusafiri kwa umbali wa karibu kilomita 20 ndani ya lori iliyokwenda kwa kasi mno na kufeli kusimama.

Alibaini kuwa hawakuwa na njia nyingine ya kutoka, isipokuwa kujaribu kutafuta njia ya kupita mji huo bila kusababisha uharibifu wa maisha ya watu na mali.

Francis Mutua ambaye ni mwenye shehena hiyo ya matofari, alipongeza juhudi ya waendeshaji boda boda na umma ambao walisaidiana kuzima moto huo ambayo ingeharibu shehena yake.