Watu wengi wanadhani huwa tunaongea na Dennis Okari - Betty Kyallo

Betty Kyalo ameweza kufichua kuwa uhusiano wake na Dennis Okari haupo hata licha ya kuwa na ushirikiano wa kuwa wazazi.

Betty ameweza kuwaambia mashabiki wake ambao ni wajasusi kuwa yeye ni mzazi mmoja anayelea mtoto wake.

Mtangazaji huyo ambaye waliweza kutengana na mume wake Dennis Okari aliweza kusema maneno hayo akiwa katika mahojiano na the Star.

"Ningependa kueka jambo hilo kama siri, labda  hivi karibuni nitaweza kusema ama baadaye, lakini kwa sasa wacha nisiliweke katika mitandao," Alieleza Betty.

Baadaye aliweza kufichua katika mtandao wake wa kijamii kwa shabiki mmoja ambaye pia ni mzazi mmoja ambaye analea watoto wake.

"Umekuwa muda sasa, vile watu pale nje wanaona jambo fulani vile liko si venye jambo hilo kwa hakika liko,

"Watu wanaeza fikiria kuwa uwa tunaongea na Okari bali hatuongei hata kidogo, anaeza kuwa hapo kwa ajili yetu ama akose kuwa hapa kwa ajili yetu, hivyo ndivyo naweza kusema," Betty alisimulia.

Akimalizia alisema kuwa yeye ni mzazi mmoja, kuwa mzazi ni jambo ambalo ni la muhimu kwa maana wakati wote unapaswa kuwa baba na mama pia.

Aliongeza na kusema kuwa hawezi ngoja aweze kukaa chini tena na mwanaume yeyote. Betty ameweze kukosolewa na mashabiki wake baada ya Okari kuoa mpenzi wa maisha yake.

Akizungumzia ukosoaji huo wakati wa mahojiano,

"Niliwacha kukasirika kwa ajili ya wanaonichukia kwa maana nilijua kila mtu anapitia changamoto zake katika maisha yao,

"Hakuna mtu yeyote ambaye ni kamili ata mimi si kamili, watu wengi huwa wananitazama kisha wananiambia wanataka kuwa na furaha kama mimi,

"Lakini hawajui kuwa huwa tunang'ang'ana ata tajiri wa matajiri pia huwa wanang'ang'ana na kupitia changamoto, na kwa hivyo niliweza kupuuza ukosoaji," Betty aliongea.

Alisema kuwa akiona jambo ambalo linamsaidia huwa analieka maanani lakini jambo ambalo halimsaidii utupilia mbali.