Watu 23, 989 wamepona virusi vya corona Afrika

Kufikia sasa, watu 23, 989 katika bara zima la Afrika wamepona virusi vya Corona huku walioaga kufikia sasa wakiwa watu 2, 355.

Aidha watu 67, 778 wanaripotiwa kuwa wameambukizwa virusi kote barani Afrika .

Kenya kufikia sasa imesaji visa 700 vya maambukizi ya virusi hivyo, huku waliopona wakiwa 251 na watu walioaga wakifikia 33.

Ulimwengu mzima, visa milioni 4.26 vimeripotiwa. Watu walioaga dunia kufikia sasa ni 287, 513 na wale waliopona wakiwa watu milioni 1.53.