Wauwaji wa Kenei walikuwa katili,' polisi watoa ripoti kuhusiana na kifo cha Kenei

Wauwaji wa askari Frank Kipyegon Kenei ambaye alikuwa mlinzi katika afisi ya naibu wa rais Ruto walikuwa werevu na waangalifu walipokuwa wakitekeleza kitendo hicho.

Polisi wanaamini kuwa Kenei aliuwawa na hakujiuwa kama ilivyo ripotiwa awali.

Wanajaribu kuchunguza vile simu ya Kenei ilitoweka baada ya kumtumia mkewe ujumbe na pia pesa.

Maafisa hao wamekuwa wakifuatilia vile simu ya mwendazake ilibadilishia eneo na kutoweka, afisa wa DCI anyechunguza mauaji hayo alifahamisha wanahabari kuwa Kenei alizungumza mara ya mwisho na mkewe saa 9/;41 Februari,18 na alimpigia akiwa nyumbani kwake.

Ni mazungumzo ambayo yalikaa dakika 53,Wakitumia teknolojia ya kisasa uchunguzi ulionyesha baada ya kumtumia mkewe ujumbe simu ya Kenei ilibadilisha eneo bali ilikuwa tu katika eneo la Imara Daima lakini si nyumani kwake.

Saa 12:25 Frebruari,19, simu hiyo lilichukuwa signal ya eneo hilo ambapo alimtumia mkewe shillingi,35,000.

“THE CHANGE IN LOCATION ESPECIALLY THE DIFFERENCE OF AT LEAST TWO-AND-HALF HOURS BETWEEN 9.52 PM AND 12.24 AM ARE CRUCIAL TIMELINESS IN PROVIDING CLUES TO WHAT TRANSPIRED." Afisa wa DCI Alieleza.

Wakati wa kumtumia baba yake shillingi,10,000 Kenei hangeweza kujibu jumbe za mkewe alizokuwa akimtumia, familia yake ilisema kuwa kutumiwa pesa hizo halikuwa jambo la kawaida kwao.

Simu yake ilizima saa 7:31 asubuhi Februari,19 na hata mitandao yake ya kijamii kutoonekana tena.

Hii ina maana kuwa walitenda kitendo hicho ili kujizuia kupatikana jinsi walitenda kitendo hicho, na wasiweze kupatikana kwa njia yeyote ile.

Inaaminika kuwa Kenei aliuwawa kikatili kabla ya kuenda kuandikisha taarifa yake kuhusiana na kesi ya sakata ya jeshi iliomkabili aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa.