Waumini wa dini ya kislamu wagadhabishwa na wizi msikitini Kakamega

Waumini wa dini ya kiislamu wameghadhabishwa na hatua ya kundi moja la vijana kuingia katika msikiti wa jamia viungani mwa mji wa kakamega na kuiba kisanduku cha pesa

Mweneykiti wa cipk kaunti ya kakamega sheikh saidi suleiman na sheikha idris mohammed wamelaani kitendo hicho

Mwisho....

Viongozi wa msikiti wa Jamia viungani mwa miji wa KAkamega wamelaani vikali kitendo ambacho kilitekelezwa na genge la majambazi kuingi katika msikiti huo na kuiba mkoba wa sadaka nyakati za usiku.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa CIPK eneo la Kakamega na Saidi Suleiman na Iddris Mohamed, wanasema genege hilo liliingia msikitini na kuiba mkoba huo uliokuwa na kiasi cha pesa kisichotambulika.

Wametoa wito kwa wazazi kuwafunza wanao maadili meme na kujiepusha vitendo potovu kama vile wizi makanisani na misikitini.

Kwingineko ni kuwa..

Polisi katika eneo la Voi, kaunti ya Taita Taveta wamewakamata wafugaji wawili baadaya ya kudaiwa kuhusika na mauaji ya mtu mmoja huko Sagalla mapema Leo baada ya ugomvi kuzuka katika ya wenyeji na wafugaji wa ngamia.

Mkuu wa polisi wa Voi Joseph Chesire anasema wawili hao ni Kati ya kundi la wafugaji kutoka eneo la Kaskazini Mashariki ambao wanazozania maeneo ya malisho na wenyeji.
Mwendazake aliaga dunia baada ya kudungwa kisu na wafugaji hao alipojaribu kuwaondoa ngamia shambani mwake.