Wawili wafariki baada ya kula maharagwe yaliyopikwa na nyanya

maharagwe (1)
maharagwe (1)

Maskini wa Mungu! Familia moja kutoka kitongoji cha Najofu kaunti ya Bungoma wanaomboleza kifo cha watoto wawili waliofariki jumamosi.

Inadaiwa kuwa, kilichosababisha kifo cha watoto hawa ni sumu iliyokuwa kwenye chakula.

Familia hii ilikula kiamsha kinywa chao kilichokuwa maharagwe na viazi vitamu ijulikanavyo kama ''Kamukhenya''.

Chakula hiki kilikuwa kimepikwa na kuandaliwa na nyanya yao ambaye hakula kiamsha kinywa chenyewe.

Babu, baba na ndugu ya waliofariki, walipelekwa kwenye hospitali ya Bungoma ambapo wanazidi kupata matibabu.

Familia hii ilipelekwa hospitalini na majirani wao.

Watoto waliofariki, walikuwa na umri wa miaka tatu na mwingine alikuwa na umri wa miaka sita.

Marehemu walianza kutapika na kuendesha saa moja baada ya kula chakula kile.

Evans Juma, baba mzazi wa watoto wale waliamka na kupata mama yake ametengeza chai na kumukhenya.

       ''Alitupa chai na kumukhenya na sote tukaila. Baadaye, mwili wangu ulianza kuwa nyonge na nikaanza kutapika.'' Juma alisema.

Baba huyu alizidi na kusema kuwa, aliona pia watoto wameanza kutapika na kukimbia chooni.

''Mtoto mmoja alizimia na tukakimbia kumpeleka kwenye Zahanati ya Bukembe. Afya ya mtoto huyu pia ilikuwa inazorota.'' Juma alisema.

Vilevile, alisema kuwa hakujua ni nini kilichokuwa kimewekwa kwenye chakula hicho ndiposa iwafanye watapike.

Nduguye Juma, Wabwile wa Barasa alisema kuwa, alipigiwa jumamosi na kuambiwa kuwa ndugu yake alienda kwa mama yao wakala chakula na wapwa wake wakafariki baada ya kula chakula hicho.

''Hatujawahi ona kitu kama hiki na hatujui ni nini kilifanyika kwani mama huwa anatupikia chakula hiki                    na hakuna siku ambayo tuliumwa na tumbo.'' Alisema.

Madaktari kutoka hospitali ya  Bungoma walipeleka sampuli ya chakula kile kwenye duka la dawa la serikali ili ifanyiwe utafiti.Wawili wafariki baada ya kula maharagwe yaliyopikwa na nyanya