Wawili Wafariki Katika Ajali Mbaya Ya Barabara Webuye

Watu wawili waliaga dunia hapo jana kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha gari aina ya Probox na Pipiki, eneo la T Junction Webuye kwenye barabara kuu ya kutoka lugulu-Webuye.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo ni kuwa gari hilo lilikuwa linaendeshwa kwa kasi likitoka lugulu kabla ya gurudumu lake kupasuka na dereva kukosa kulidhibiti.

Gari hilo liligonga muhudumu wa pikipi na kupelekea kifo cha dereva na muhudumu huyo wa pikipiki papo hapo

Hata hivyo wakaazi wa eneo hilo wamelalamikia ongezeko la visa vya ajali kwenye barabara hiyo.

Aidha wametaka serikali kuingilia kati na kuweka matuta kwenye barabara hiyo ili kuzuia maafa zaidi.

-Brian Ojamaa