Wazazi ni miongoni mwa washukiwa wakuu wa watoto waliopatikana katika kituo cha polisi

children-killed
children-killed
Wazazi wa watoto wawili waliopatikana katika kituo cha polisi cha Athi River wiki jana wakiwa wamefariki ni miongoni mwa washukiwa wakuu wanaochunguzwa na DCI.

Makachero kutoka DCI wamewahoji watu kadhaa katika eneo ambalo miili ya watoto hao ilipatikana ikiwemo mhudumu wa Canteen katika kituo hicho cha polisi.

Taarifa kutoka DCI sasa zinasema kuwa wameanza kuchunguza namna watoto hao walitoweka huku wakimchunguza mzazi mmoja.

Kulingana na polisi, huenda wazazi hao wanajihusisha na maswala ya ushirikina na labda wanahusika pakubwa kutokana na kupotea kwa watoto hao na hata kifo chao.

Wanasema walishangazwa namna miili ya watoto hao ilikuwa imepangwa huku mvulana akiwa uchi, swala ambalo linawafanya kuanza kuwachunguza wazazi hao.

 Taarrifa zingine zinadai kuwa huenda mauaji hayo yalifanyika kama njia ya kutoa kafara.

“There is crucial information which makes detectives believe the couple has a case to answer. From preliminary investigations into the cruel death, the incident might not have just been cruelty but a heinous act targeting a beneficial outcome,”