Mama.G.1

Wazazi walinipeleka jela walipojua mimi ni shoga – Mama G

Phelix Kasanda almaarufu, ‘Mama G’ ambaye ni shoga ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni.

Phelix ambaye alizaliwa katika familia ya watoto 6, anasema kuwa alizaliwa na hisia za ushoga na aliishi kujifungia na zile hisia hadi alipoamua kutangaza miaka tisa iliyopita. Hata hivyo alikiri kuwa hawezi walaumu wazazi wake.

ILIKUAJE: Sababu yangu ya kumficha baba mtoto – Jackie Vike (Awinja)

Kulingana na Mama G, pindi tu alipowajulisha wazazi wake kuwa yeye ni shoga walimpeleka rehab, wakampeleka aombewe kabla ya kumpeleka jela ambapo alikaa kwa miezi kadhaa, ili abadilishe tabia.

Mama.G

“Hakuna aliyeniingiza kwa ushoga na naonelea ni hisia niliyozaliwa nayo. Ukiwa unalelewa kama mwanaume na kwa jamii huwezi jisema kuwa wewe ni shoga kuepuka aibu.” Alisema Mama G.

Aliongeza,

Nimezaliwa familia ya watoto 6 kutoka Kisumu na nililelewa vizuri bila tatizo, venye nimelelewa imechangia mimi kuwa shoga na sitaki kuwalaumu wazazi wangu.

ILIKUAJE: Nilipoteza kidole changu nikitafuta utajiri – Nelson Namanda

Je mamake aliipokelea aje habari hiyo?

Sio rahisi mama mzazi kukubali mwanawe ni shoga na analala na wanaume wenzake kwani kuna siku walinipeleka rehab, maombi na pia nikawekwa cell ili nibadilike.

Alisema kuwa akiwa na miaka 25, alifungiwa kwa miezi mitatu na haikuwa rahisi kwani mle ndani watu hutaka kujua sababu yako kufungiwa na aliposema sababu, wafungwa wengine walitaka uhusiano naye.

Katika pilkapilka ile alianzisha uhusiano na jibaba mzee humo ndani kwani alikuwa anamchunga na pia kumpa chakula.

Ilikuaje: Nilizaliwa kijana lakini sasa mimi ni mwanamke – Audrey Mbugua

Mama.G.000

Je yeye hupatana wapi na shoga wenzake?

Mimi hupatana nao kwa mitandao ya kijamii kwani watu wako wengi na unapata kila mtu ana taste yake, kwa mfano mie napenda vijana barobaro mwenye ameunga kidogo.

Mimi katika uhusiano huwa ‘bottom’ au mwenye ana behave kama mwanamke katika mahusiano.

 

Cha kushtua ni kuwa kuna siku mama G alinajisiwa akiwa anaelekea nyumani usiku mmoja na kwa uwoga wa kuanikwa, hakuripoti kisa hicho kwa polisi.

Nilikuwa nimetoka out usiku naelekea nyumbani na kuna zile mogoka zone na kuna mavijana walikuwa hapo, waliniita na wakasema kuwa watanionesha na hapo wakaninajisi.

Cha kushtua ni kuwa licha ya kudhulumiwa hakuripoti kwa polisi kwani alihofia kushikwa na kufungiwa au pia kuanikwa kwa vyombo vya habari. 

Photo Credits: Stephen Manjala

Read More:

Comments

comments