Wazazi wangu waliachana nikiwa na miaka kumi-Mercy Kyallo

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Mercy Kyallo dada yake Betty Kyallo, uvumi umekuwa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wamekosana.

Betty alipokuwa akizindua saluni yake dada yake Mercy hakuhudhuria hafla hiyo kwa maana kuna ugomvi kati yao.

"Betty amechangia katika umaarufu wangu katika biashara yangu, nilipofutwa kazi nilikaa nyumbani miezi miwili nikiwa na mawazo chungu nzima

Wakati wa kufutwa kazi nilikuwa na mpenzi ambaye alinipa ushauri na kunitia moyo sana." Alieleza Mercy.

Alipoulizwa kuhusu baba yake alikuwa na haya ya kueleza,

"Nakumbuka baba yangu alienda ulaya kutafuta kazi nikiwa na miaka kumi, hapo ndipo waliachana na mama yangu kusema ukweli tulisumbuka sana lakini namshukuru Mungu kwa maana ametuwezesha

Baba yangu yuko hai na huwa tunazungumza licha yake kuachana na mama yangu."

Miezi michache iliyopita Mercy alikejeliwa sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumkashifu rafikiye aliyekuwa mume wake Betty Kyallo, hii ni baada ya mwanawe betty Ivanna kulazwa hospitali kwa muda.

"Kwa kweli sikuwa nimemkashifu Baba yake Ivanna bali alikuwa rafiki yake kwa kuingilia mambo ya familia sana, baada ya kukejeliwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii niliumia sana

Jambo ambalo liliniuma wakati huo ni mmoja wa mashabiki aliponiambia nipambane na hali yangu na niache ya wengine yaani 'i should mind my own business." Alizungumza Mercy.

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao yetu ya kijamii ya youtube.