Waziri Matiang'i ahidi kusafisha usafirishaji wa kitaifa na mamlaka (NTSA)

Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i ameahidi kusafisha sekta ya usafirishaji wa kitaifa na mamalaka ya usalama na kuondoa wafanyakazi ambao hawana muelekeo.

Alisema kuwa wametambua mapungufu mengi ambayo yanayo sababisha shughuli ambazo hazifai katika shirika hilo.

"Tunaenda kusafisha kabisa na kurekebisha NTSA na kuhakikisha kuwa shirika hili linafanya mambo ama shughuli ambazo zinastahili," Matiang'i alieleza.

Matiang'i alisema kuwa shirika hilo limevunja kanuni na sheria nyingi kwa sababu ya mianya ambayo ikokatika muundo.

Shirika hilo awali lilikuwa katika huduma ya usafirishaji kisha kupelekwa katika huduma ya mambo ya ndani.

Januari 21 mwaka huu Rais Uhuru Kenyatta alimpa waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i mamlaka mingi, akisema kuwa hatua hiyo itasaidia kazi kufanywa kwa njia ipasavyo.

Wanachama wapya ni, Jane Obwacha, Catherine Waweru, Alice Chesrire, Francis Mwongo, Moses Gachemi na Meshak Kidenda.

Si gari tu ila wanabodaboda wengi wamelalamika kuhusu kupewa namba sawa na za pikipiki nyingine.

Ijumaa iliopita maafisa 6 wa NTSA walishtakiwa kwa kupeana namba ya gari sawa na iliotekeleza shambulizi mwezi jana. Anthony Kadu, Jacqueline Githinji, Cosmas Ngeso, Irvung Irungu, Stephen Kariuki na Charles Ndung'u walifikishwa mbele ya hakimu mkaazi mwandamizi Caroline Nzibe.