Waziri Tobiko asema Ruto ni karani wa Uhuru na kumtaka Murkomen kuheshimu rais

TOBIKO
TOBIKO
Sasa ni wazi kwamba kuna tofauti kali baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Hii ni baada ya waziri wa mazingira Keriako Tobiko kumtaka Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na 'mkubwa wake' kuheshimu rais.

"Huyu mkubwa wake ni karani ya rais...na vile mimi na mheshimu rais hata huyo deputy na huyo Murkomen wamheshimu rais," Tobiko alisema.

Tobiko siku ya Ijumaa alisema kwamba inasikitisha kuwa Murkomen anafikiri kuwa yeye pekee ndiye aliye na uwezo wa kutusi kila mtu akiwemo rais.

Soma habari zaidi;

Waziri alikuwa akijibu matamshi ya Murkomen aliyemuita karani katika serikali ya Jubilee na amabye hangepata kazi kama si kwa juhudi za naibu rais William Ruto aliyemsaidia rais Kenyatta kuunda serikali.

https://twitter.com/i/status/1301964491362570240

"Unasahau haraka kwamba ulipata uaziri kwa sababu rais alitaka kukuondoa kutoka ofisi ya DPP. Hauna mamlaka kimaadili kumsomea naibu rais hata kama anadhulumiwa na mkubwa wake. Kwanza jaribu kuwa MCA," Murkomen aliandika kwenye twitter.

Lakini Tobiko akihudhuria hafla katika msitu wa Loita kaunti ya Kajiado alimkaripia Murkomen akisema kwamba hana heshima kwa watu wengine.

"Kuwa Murkomen awe na dabu manake hana adabu kabisa. Amekuwa yeye ni wa kuongea na kutukana viongozi wengine hata rais. Lazima aambiwe awe na adabu na kumheshimu rais. Hata huyo Mkubwa wake ni karani wa Rais. Alisema Tobiko.

Soma habari zaidi;

Waziri Tobiko aliongeza kwamba heshima ina pande mbili na ikiwa Murkomen na naibu rais hawataheshimu rais basi wao pia hawastahili kuheshimiwa na yeyote.

Tobiko alisema kwamba Murkomen alikuwa amechochea jamii katika msitu wa Mau kukaidi agizo la rais kuondoka msituni.

Murkomen katika ujumbe wake wa twitter alisema kwamba kawaida kwa kumkosea heshima naibu rais Tobiko angekuwa amepigwa kalamu na rais lakini ni kama anaungwa mkono na rais kudunisha naibu wake.