Waziri wa Elimu Amina Mohammed akabiliwa na maswali ngumu

sos
sos
Waziri wa elimu Amina Mohammed akabiliwa na maswali magumu bungeni kuhusiana na mtaala mpya wa masomo.

Wabunge walitaka waziri Amina kuwaelezea kwa kina kwanini mtaala huo mpya haungeendelea na kisha baadaye kubadili msimamo wake siku chache baadaye.

Majira ya saa tano Alhamisi  Amina alifika katika kikao, Kipsang na wabunge wengine wa wizara hiyo ili kuweka wazi masuala kadhaa kwanini walibadilisha mtaala mpya,

Wabunge walimtaka kuelezea kwanini aliwapotosha wazazi wengine kwa kusema mtaala huo umeahirishwa kisha kupinga kauli hiyo

"Hatupaswi kupeleka nchi katika safari isiyojulikana, ni rahisi kusema kuliko kufanya kama huduma mnaweza kushawishi nchi kuwa mna tathmini tosha" William Sossion alisema.

Wabunge pia walitaka kujua kwanini vitabu vya mtaala mpya viko shuleni ilhali si mtaala huo unatimika katika mashule. Mkurugenzi mkuu wa mitaala nchini KICD Dkt Julius Joankuweka bayana kauli hizo.