yusuf juma

Wazo La Siku Naye Yusuf Juma, Mechi 28, 2017

Kinaya cha bei ya unga wa ngano kuzidi bei ya Unga wa mahindi.Ubaradhuli wa Idara zote za serikali kuharibu pesa za umma kumchuguza gavana mmoja ilhali Mabilioni yaliofujwa hayajulikani yaliko.Udhaifu wa fikra zetu kusifia na kutetea uongozi usiojali unkula lini na unkula nini.Upuuzi wa kundi kubwa lenye maamlaka ya kuleta mageuzi(vijana)kuzongwa na yasiofaa.Masikitiko ya ahadi kutibuliwa na kuwa nyimbo za takwimu zisizotusaidia. Utepetevu usiokadirika wa raslimali zote kufujwa na kufurika mifuko ya wachache.Ukatili mkubwa kwa familia zisizojimudu baada ya maelfu ya kazi kupotea .Huruma isiokadirika kwa wakulima wasioweza kulipa karo kwa kipato cha mazao ya jasho lao.UJINGA mkubwa wa kukubali hali ya kuwa Waaathiriwa na kuitikia kugawanywa kikabila.Tuamkeni!

Photo Credits: yusuf

Read More:

Comments

comments