WEBUYE: Mwanaume mmoja amuua mwanafunzi kabla ya kuuliwa na umati

mauaji
mauaji
Mwanaume mmoja kutoka kijiji cha Maram wadi ya Matuli kwenye eneo bunge la Webuye Magharibu usiku wa kuamkia leo amemuua mwanafunzi wa darasa la nane wa shule ya msingi ya kutwa ya Lugulu kwa sababu isiyojulikana na kabla ya kuuawa na wananchi wenye adhabu.

Kulingana na babake mwanafunzi huyo mzee Samson Simiyu Toroi ni kuwa mwanawe alikua ametoka safari Kisumu, na wenzao na alikua anarejea chumbani mwake ambapo alivamiwa na jirani yake kwa jina Kadenge aliyemkata shingo na alipokimbizwa katika hospitali ya kamisheni ya Lugulu alikuwa tayari ameaga dunia.

Mzee Toroi amehoji kuwa hajawai kusikia kuwa mwanawe amemkosea Kadenge kwa njia yoyote na alishangaa na kisa cha jirani yake.

Hata hivyo nduguye marehemu ambaye alielekea kwa Kadenge kuuliza sababu ya kumuua nduguye pia alivamiwa na kukatwa panga kifuani na anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kamisheni ya Lugulu.

Kisa hicho kiliwagadhabisha wakazi waliovamia boma la yule aliyemuua mwanafunzi huyo.