Wee! Tazama jumba ambalo Size 8 amejiweka chini ya karantini kufuatia hofu ya Corona

DJ-Mos-new-home
DJ-Mos-new-home
NA NICKSON TOSI

Picha zinazoonyesha kasri la Size 8 na mumewe DJ Mo zimewaacha wengi vinywa wazi, haswa sebule ya nyumba hiyo ambayo imepambwa kwa viti vya kisasa, viti ambavyo viliwaacha wengi wakitokwa na mate ya tamaa.

DJ Mo anaendelea kuwa chini ya karantini baada ya kuwasili nchini  hivi karibuni  kufuatia agizo la serikali kuwa kila mtu anayewasili nchini ni sharti kujitenga na watu kwa siku 14 ili kubaini iwapo ameambukizwa virusi vya Corona.

Akinakili video ya mumewe akiwa pekee yake kwa nyumba hiyo, Size 8 aliandika hivi.

Ushawai kuwa chini ya karantini mpaka unafikiri kubadili viti  😂😂😂😂😂umeketi chini hadi kuzoeana na kiti 😂’aliandika Size8

katika video hiyo nyumba hiyo haswa sebule inakaa kubwa kuliko baadhi ya nyumba jijini Nairobi kwa jina Bedsitters.

Hizi hapa ni baadhi ya picha hizo.

The Murayas kama wanavyofahamika na mashabiki wao inasemekana walihamia kwa nyumba hiyo iliyoko Lavington mwaka jana .

Wakati wa ununuzi wa nyumba hiyo, tumebaini kuwa walilazimaka kutoa kati ya milioni 45 na 80 ili kuwa wamiliki rasmi wa kasri hilo.