Wema Sepetu atimka mbio baada ya kutoka gerezani Segerea

Wemapic
Wemapic
Malkia wa filamu nchi jirani ya Tanzania Wema Sepetu ametimua mbio kutoka gereza la Mahabusu Segerea baada ya mahakama ya Mkazi Kisutu kumwachilia huru. Wema alikuwa amefungwa rumande kwa kipindi cha  siku 7 akisubiri maamuzi ya dhamana ya kesi mbili zilizomwandama.

Soma hapa:

Kesi ya kwanza ikiwa ya kuusika na dawa za kulevya na zaidi ya hapo kuchapisha picha za kufedhehesha za ngono katika mtandao wa kijamii. Hali kadhalika Wema alikuwa amefungwa baada ya kususia vikao viwili ya mahakama hiyo.

Aunty Ezekiel, mamake Diamond Platnumz na Esma Platnumz ni kati ya mastaa na ambao walikesha kumuombea nyota huyu akiwa gerezani. Maira Kasonde ametoa tahadhari kubwa kwake endapo atakiuka masharti aliyowekewa ya dhamana.

https://www.instagram.com/p/By4frejgnRh/

Mwanzoni wa juma lililopita, habari za staa huyu kufungwa rumande zilizagaa katika vyombo vya habari. Wema alijitetea kuwa kutofika mahamakani kulichangiwa na kuumwa na tumbo kutokana na hedhi zake.

Soma hapa:

"Mahakama hii inatoa onyo la mwisho kwa mshtakiwa, ikitokea mshtakiwa huyu amevunja sheria ya kutofika mahamakani bila taarifa, mahakama hii haitasita kumfutia dhamana." alitoa amri Jaji Maira Kasonde.

Maira ameamarisha kuwa Wema ameachiliwa huru kwa dhamana na kuwa ushahidi dhidi yake utatajwa tarehe 14 Julai mwaka huu .