'Wenger Asipoenda Tutamtumia Nyuki Emirates' - Gidi

Bwana Gidi alirudi studioni rasmi siku ya Jumatatu baada ya kufanya utangazaji kwa mda mfupi siku ya Ijumaa baada ya kurudi kutoka kwa likizo yake ya takriban majuma mawili.

Mtangazaji huyo ambaye alikuwa ameahidi mashibiki wa Redio Jambo kuwa atasafiri kwanza hadi uga wa Emirates uga wa timu ya kadanda ya Arsenal, huku nia yake kuu ikiwa kumshurutisha kocha Arsene Wenger aondoke klabu hiyo baada ya miaka nyingi ya kutoshinda taji la ligi kuu.

Na kama alivyoahidi, alitembelea afisi za Wenger lakini hakubahatika kumpata ila alipewa fursa ya kuzungumza naye kupitia rununu.

Huku akisimulia jinsi mazungumzo yake na bwana Wenger yalivyofanyika, Gidi alifichua kuwa kocha huyo alituliza roho yake kwa kumpa mwaliko maalum kutizama mechi kati ya Arsenal na Bournemouth, ugani Emirates.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be