Weta ataka benki kuu kuhamasisha umma juu ya sarafu mpya

Kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula ameitaka benki kuu nchini kuweka mikakati ya kuwahamasisha umma kuhusu vipengee vya salaama vya sarafu mpya ili kuzuia noti bandia.

Akizungumza katika eneo bunge la Kabuchai wakati wa zoezi la uchaguzi wa chama cha Ford Kenya, Wetangula amesema ipo haja ya benki kuu kubadilisha sarafu hiyo kwa haraka ili kuepukana na wahalifu ambao huenda wakatumia

nafasi hiyo kuwapora wakenya.

Wito huo umeungwa mkono na mbunge wa Kabuchai James Mukwe.

Kwingineko ni kwamba

Wazazi katika kaunti ya kakamega wameunga mkono mfumo mpya wa serikali wa kuchagua halmashauri za shule na pia kutoa mwongozo wa usimamizi

Wakiongea katika shule ya msingi ya shikoto mixed kwenye warsha ya uzinduzi wa bodi za shule za msingi wazazi hao ambao wamechaguliwa kusimamia shule wamesema mfumo mpya umewapa changamoto ya kuona kwamba wanawajibikia elimu bora katika shule