rsz_moses-wetangula

Wetangula Awasuta Wapinzani Wake Kuhusu Azma Yake Ya Urais

Seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetangula amewakashifu wapinzani wake kwa kudai kuwa analenga kusambaratisha mrengo wa CORD na azma yake ya kuwania kiti cha urais.

Wetangula alisema kuwa azima yake ya kuwania urais akiwa ndani ya mrengo wa CORD ni ishara tosha kuwa mrengo huo unadumisha demokrasia tofauti na mrengo wa Jubilee.

Aliongezea kuwa madai ya wapinzani wake isiwapotoshe wafuasi wa CORD huku akisisitiza kuwa azima yake inalenga kulinda kura za eneo la magharibi.

Aidha haya yanajiri baada ya baadhi ya wanasiasa kutoka eneo la Nyanza kudai kuwa Raila Odinga hapaswi kumuunga Wetangula mkono kama mgombea urais kupitia tiketi ya CORD.

 

wetangula

Photo Credits: files

Read More:

Comments

comments