Wewe ni sura mbovu ya kutojali Ruto kwa Raila juu ya kashfa ya mabwawa

Ni vita ya maneno ambayo ilizidi unga na kitumbua kuingia mchanga wakati naibu wa rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga walijibizana kwa maneno kwa sababu ya kashfa ya mabwawa.

Maneno yalizidi hadi pale Ruto aliweza kumuita Raila kuwa yeye ni sura mbovu ya kutojali.

Ruto aliweza kusisitiza kuwa anajua pesa ambazo zimetumika katika mabwawa hayo kwa sababu yako katika manifesto ya Jubilee.

Naibu wa rais aliweza kumtuhumu aliyekuwa waziri mkuu Raila kwa kupiga siasa vita dhidi ya rushwa huku akisema...

"Wewe ni sura mbovu ya kutojali na mwanasiasa mdanganyifu anaye julikana na maneno yake ambayo haya maanishi kitu chochote." Aliongea Ruto.

Alisema kuwa Raila ni mwenye sifa mbaya na muongo na mtu ambaye hawezi kukumbuka uongo wake wa mwisho.

Ruto hakuweza kutia kikomo bali aliendelea na kusema kuwa vita ya rushwa itaweza kukamilika vyema kama itaweza kupigana na ukweli na vifaa vi vaavyo.

Alisema kuwa hana uhalali wala uadilifu wa kumsomea mtu kuhusu rushwa na uadilifu.

"Ndio nina nia ya ujenzi wa mabwawa hayo  kwa sababu pamoja na rais Uhuru Kenyatta tuliweza kueka mradi wa mabwawa 57 kujengwa miaka hiyo mitano." Ruto alisema.

Aliongeza na kusema kuwa."Kama naibu wa rais wa serikali ya Kenya, ningeanguka kama singefuatilia idadi hiyo." Aliongeza Ruto.

DCI anafanya uchunguzi kuhusiana na madai kuwa billioni 21 zimepotea za mabwawa ya Arror na Kimwarer katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Ruto yuko katika rekodi huku akisema kuwa hakuna fedha ambazo zimepotea wacha tu billioni 7 ambazo ziliweza kulipwa mkandarasi kwa mapema.

"Kwa hivo swali ambalo naulizwa ni kama fisi kumuulizwa mchungaji, ni nini hasa nia yako katika kuchunga, na kwanini unajua idadi ya mifugo ambayo uko nayo." Ruto alizungumza.

Aliongea maneno hayo Alhamisi katika mkutano wa kufunga 6th Devolution Conference kaunti ya Kirinyaga.

Katika eneo hilo ndipo bado kinara wa ODM Raila aliweza kukashifu na kusema Ruto hapaswi kutetea fedha za mabwawa hayo kama anajua mzuri hajui mahali fedha hizo zilikoenda.

Raila aliweza kuuliza swali imekuaje Ruto anajua ni billioni 7 pekee ambazo zimeweza kupotea.