Wewe toroka tu,Tutakufuata hata Kaburini- Mutahi ataka Jamaa aliyetoroka Mbagathi kujiwasilisha

unnamed (6)
unnamed (6)
Serikali sasa inataka mgonjwa aliyetoroka kutoka kwa hospitali ya mbagathi baada ya kuwekwa chini ya karantini kujiwasilisha yeye mwenyewe. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema japo mgonjwa huyo ana uwezo wa kujificha, serikali itafanya vyovyote vile kuhakikisha kuwa amepatikana na kuchukuliwa hatua.

Mapema wiki hii, kuliripotiwa kuwa mgonjwa huyo mwanamme alitoroka hospitali hiyo baada ya kuwatishia madaktari na hata bawabu kwa kisu.

Mutahi kwa upande wake alisema wizara yake haijapokea taarifa hizo japo akasema uchunguzi utaanzishwa mara moja.

"I want to appeal to this person: Please come back. Where are you running to? Your home, your wife or mother... Why are you risking the lives of others," Kagwe alisema

Amesema kuwa baadhi ya watu waliokuwa wanakimbia kutoka kituo cha Mbagathi wenyewe wamekuwa wakijiwasilisha baada ya kubaini kuwa ni wagonjwa.

"Even of you run, I want to assure you that we shall find you. The long arm of the law will catch up with you". Alisimulia Mutahi.

Taarifa hizi zinajiri huku Kenya ikiendelea kuandikisha visa vingi vya maambukizi na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa nchini kuwa 1618.

Wakati uo huo majimbo 32 kati ya 47 nchini sasa yameandikisha visa vya maambukizi ya virusi hivyo huku kaunti za hivi karibuni zikiwa Nyeri na Uasin Gishu .

Kenya kwa sasa imewapima watu 70,172 kuhusiana na virusi hivyo.