What? Kikao cha bunge chakatizwa baada ya picha za ngono kuibuka

Bunge la kitaifa la Afrika Kusini lilifunga bunge kufuatia mlipuko wa virusi vya corona. Wabunge kwa muda sasa wamekuwa wakifanya vikao vyao kupitia kwa njia ya mtandao wa kijamii.

Kikao ambacho kimekuwa kikifanyika kupitia mtandao wa kijamii wa zoom, kilikatizwa baada ya picha ya ngono kujitokeza kwenye skrini.

Spika Thandi Modise alighadhabishwa na picha hizo huku akisema hiyo ni sababu kuu ambayo humfanya apinge mikutano ya mitandaoni.

Imeripotiwa kuwa, wahandisi wa bunge hilo walilazimika kutumia kiunganishi kingine ambapo wabunge waliungana tena na kuendelea na kikao chao.

Kwa mujibu wa tovuti ya EyeWitness, Wabunge walitaja tukio hilo kuwa la aibu na la kukera sana.

Kwa sasa, bunge la Afrika Kusini limefungwa na vikao vyote vinafanyika kwa njia ya mitandao huku nchi ikiendelea kukabiliana na jinamizi la ugonjwa wa corona.