Who’s Next? Baada Tanasha Diamond atamnyakua nani?

Chibu kama anavyojulikana Staa wa  muziki wa Bongo Diamond Platinumz ametamba sana  kwa ajili ya muziki wake mzuri na wa kuvutia.

Nyota huyo hata hivyo pia amegonga vichwa vya habari kwa msururu wa vidosho ambao amehusiana nao na kisha kuwaacha hoi kila anapopata mpenzi mwingine. Diamond sio mgeni kwa sakata na amepata umaarufu sana wa kuweza kukana madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake kadhaa nchini Tanzania. Hawa hapa ni baadhi tu ya wanawake wanaojulikana kuwahi kuwa na uhusiano  na Diamond ingawa amekuwa akikana kuhusika katika mahusiano yoyote na baadhi yao.

Zari Hassan

Mapenzi kati ya Diamond na Zari yalishika kasi  kuzungumziwa kote Afrika. Walikuwa  kilichotajwa kama   ‘The altimate power Couple’ na kila mtu alitaka kuwa kama wao. Diamond alikuwa katika kilele cha taaluma yake ya muziki na Zari amefahamika sana kwa  mafanikio yake katika biashara.Kiliingia mchanga kitumbua chao wakati Zari alipoushangaza ulimwengu kwa kudai kwamba Diamond alikuwa na uhusiano wa nje ya ndoa yao.  Diamond na Zari walifanikiwa kupata watoto wawili  Latifa Dangote na  Prince Nillan.

Hamisa Mobetto

Uhusiano wa Hamisa na  Diamond  umeghubikwa katika usiri mkubwa lakini matokeo yake yamekuwa uvumi mrefu na sakata ya mara kwa mara.  Kilichofichuka baadaye ni kwamba wawili hao wana mtoto  Dylan. Hamisa aliwahi pia kujitosa katika muziki lakini  hakuweza kupata mafanikio kama ya Diamond .

Tunda Sebastian

Tunda ni  staa mwingine wa Tanzania ambaye amehusishwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond. Kipusa huyo ana urembo wa kuvutia na huwezi kumlaumu Diamond kwa kujipata katika mikono yake na cheche za mahaba ya  mrembo huyo.

Wema Sepetu

Wema Sepetu  imeripotiwa alikuwa mpenzi wa Diamond kwa muda mrefu  na imekuwa vigumu sana  kwake kujiondoa kabisa kutoka maisha ya msanii huyo. Wawili hao awali walikuwa wakionekana pamoja lakini katika siku za hivi karibuni, hawajakuwa wakitangamana kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita .

Shaddy Boo

Kipusa huyu mnyarwanda  ilidaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond kisiri lakini kwa  sababu mapenzi ni kama kikozi, hayawezi kufichika, baadaye yote yalijulikana. Wakati Fulani aliwahi kuweka picha mtandaoni  akisema alikuwa ametekwa kabisa na mapenzi kwa msanii huyo .

VJ Penny

Muimbaji Penny alikuwa mpenzi wa zamani wa Diamond  na hata walikuwa wamepanga kufunga ndoa mwaka wa 2013 kabla ya  mambo kutibuka. Inaaminika wana mtoto lakini pia kuna uvumi kwamba huenda wawili hao wana ujamaa na hivyo basi kufanya kuwa vigumu wao kuonekana .

Tanasha Dona

Tanasha ndiye  wa hivi punde kutengana na Diamond  ingawaje watu wengi bado hawajaamini kwamba Diamond ameachana na  Tanasha  baada ya kutoa wimbo wao pamoja hivi karibuni . Jumbe anazotuma Tanasha katika mitandao ya kijamii zinaashiria kwamba huenda penzi lao liliingia mchanga .Je ni yupi sasa atakayefuata katika orodha ya msururu wa wapenzi wa Simba?