Wicked Family! Jinsi Diamond na familia yake ilivyomhadaa Tanasha kwamba yeye ndiye Tosha

Uhusiano wa Diamond Platnumz  na Tanasha  ulikumbwa na kisirani kuanzia mwanzo kwa sababu pindi tu ilipofichuka kwamba wawili hao ni wapenzi, watu walitabiri kwamba uhusiano huo haungedumu.

Tanasha  alianza mahusiano na Diamond  Oktoba mwaka wa 2018  miezi kadhaa baada ya kuachana na  mpenzi wake. Diamond aliliandika jina la Tanasha katika bichi na kuposti picha hizo kwenye instagram, muda mfupi baadaye Tanasha alikuwa na watu wengi waliomfuata katika instagram.

Kabla ya kufahamu kinacho msubiri mbele, Tanasha alikuwa ashajiingza katika lindi la mapenzi na msanii huyo.

 MAMBO YALIANZA KWENDA MBIO. SIKUWA NIMEMPENDA WAKATI HUO. NILIPENDA UKAKAMAVU NA MSUKUMO WAKE.

Sasa baada ya kutengana kwao, inadhihirika wazi jinsi Diamond na familia yake walivyomhadaa Tanasha na kisha kumuacha

1.  kutangaza tarehe ya harusi

Miezi mitatu baada ya kuanza kwa uhusiano wao, Diamond  aliharakisha mambo na kutangaza kwamba wangeona na Tanasha Februari mwaka wa 2019, lakini hilo halikufanyika.

… GHAFLA AKATAKA KUNIOA. HII ILIKUWA BAADA YA MIEZI MITATU YA KUHUMBIANA ,TAREHE IKAAMULIWA KUWA FEBRUARI

Aliongeza ;

 NILITAKA KUTUMIA MUDA WA KUTOSHA ILI TUJUANE IFAAVYO

  Diamond aliendelea kuahirisha tarehe ya harusi yao na mojawapo ya kisingizo kilikuwa kwamba mamake Tanasha alikuwa ameishi bara ulaya na hakuwa amepata likizo ya kuja kuhudhuria harusi ya binti yake.

2.  Kumlimbikizia mapenzi tele tele

Msanii huyo wa bongo alihakikisha kwamba Tanasha anapata starehe zote kabla ya kujua kilichokuwa kikimngoja.

‘  Chipukizi na  mpole’ hivyo ndivyo familia ya Diamond ailivyokuwa akimuita Tanasha ili kuwapandisha mori wapenzi wake wa zamani Zari na Hamissa.

3.  Kucheza na akili zake

Waliutoa wimbo pamoja huku Tanasha akimuomba Diamond asimuache au kucheat. Kwa mistari hiyo Simba alijibu;

EEEH! MAMA KASEMA MWALI MWANA

NIMEPATA NITULIE SIMBA

OH NITULIE SIMBA

OH NITULIE SIMBA

ZILE CHENGA VIDANGA DANA

VICHECHE NICHUNIE SIMBA

OH NICHUNIE SIMBA

OH NICHUNIE.

Lakini hata kabla ya mwezi mmoja  kutamatiika  baada ya kuutoa wimbo huo, walitengana

4.  kukanusha kuwa  na mpenzi wa kando

Diamond amekuwa akicheat wakati yupo katika mahusiano na wanawake wote waliomzalia lakini kila mara madai yalipozuka alikanusha vikali.

Katika mahojiano na TRUE LOVE  Tanasha amesema uhusiano wao ulianza kupata zogo miezi sita kabla hawajatengana.

FOR THE PAST SIX MONTHS, WE WERE STILL TRYING TO SEE HOW WE COULD MAKE THINGS WORK AND THEN IT GOT TO A POINT WHERE YOU FEEL LIKE THE OTHER PERSON HAS JUST LOST INTEREST AND IT’S NOT BECAUSE OF ANYTHING EMOTIONAL I WOULD SAY IS NOT LIVING UP TO CERTAIN EXPECTATIONS HE HAD IN THE RELATIONSHIP. IT’S NOBODY’S FAULT,’  alisema

Tanasha amesema alichoka na usinzi wa Diamond na kuamua kuondoka .

I COULD FIGHT ALL THOSE PEOPLE BUT I REALISED I COULDN’T FIGHT ALONE. MY MOM HAS SHOWN ME THAT IF IT DOESN’T WORK, YOU FIGHT. IF IT IS TOO MANY BACK AND FORTH OR WHEN YOU REACH A DEAD-END THAT IS WHEN YOU BOUNCE. I FOUGHT IT ALL. BUT WHEN IT CAME TO INFIDELITY I REALISED I WAS FIGHTING A WAR ON MY OWN.

Lakini kabla ya kuondoka, Tanasha wakati wote alikuwa akimtetea Diamond

5.  mapenzi feki kutoka kikosi kizima cha Wasafi na familia ya Diamond

Tanasha alionyeshwa mapenzi na familia ya Diamond na hata hawakuficha kwamba sasa ndiye ambaye Simba angeamua kufunga naye pingu za maisha. Esma, dadake Diamond ndiye aliyenza kwa kumsifu kwa ukomavu kuwaliko wapenzi wa awali wa Diamond.

Mapenzi yao kwake yalizidi walipogundua kwamba birthday yake ilikuwa siku moja na ya mamake Diamond- Julai tarehe 7.

Karamu kubwa ya birthday iliyounganishwa iliandaliwa na kuhudhuririwa na wasanii tajika wa Bongo. Mama Diamond alimsifu sana mkaza mwanae mtarajiwa lakini yote yalitumbukia nyongo pindi tu alipojifungua.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO