William Samoei Ruto atarajiwa kuzuru ngome ya kinara wa ANC Musalia Mudavadi

Naibu wa rais William Ruto anatrajiwa kuzuru kaunti ya Vihiga leo jumamosi. Ruto atarajiwa kuhudhuria hafla ya wamama itakayofanyika maeneo ya Nabwani katika eneo bunge la Sabatia.

Wachambuzi wa siasa wanahoji kuwa hii ni njama fiche ya ya kupenyenza katika ngome ya kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi. Ruto na Mudavadi watakuwa wanapimana nguvu katika zoezi la upigaji kura eneo bunge la Kibra. Wawili hawa tayari washapendekeza majina ya wawaniaji wao.

Soma hadithi hapa;

Eliud Owalo wa chama cha ANC atakuwa anamenyana na Mariga ambaye vyanzo mbalimbali vinahoji kuwa alipendekezwa na naibu wa Rais. Aidha wawili hawa watakutana na mgombeaji wa ODM atakayetangazwa mshindi katika mchujo unaofanyika kwa sasa.

Ikumbukwe kuwa wiki mbili nyuma Ruto alikuwa katika maeneo ya Luanda katika hafla aliyoalikwa kama mgeni wa heshima . Safari hizi za naibu wa rais zinaonekana kuwa na azimio kubwa la kumfanya aoenekane "Jirani Mwema" ili mwaka wa 2022 apate uungwaji mkono katika eneo hili tajiri sana kwa kura.

Soma hadithi hapa;

Vyanzo mbalimbali vimenukuu wandani wa Ruto wakihoji kwamba wapiga kura wajitahidi sana kuwalaki viongozi kutoka jamii tofauti bila ubaguzi. Je, huenda Ruto kapania kuwateka wapiga kura katika jamii ya Mulembe?